BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

Kikao cha Baraza la Madiwani kimefanyika tarehe 4 Novemba 2021 huku kikihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Alexander Mahawe. Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mh. Joseph Nyambwe kilijadili mambo mengi yakiwemo kupandisha mapato ya Halmashauri. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma aliwasihi viongozi wenzake kuzidi kujifunza kutoka Halmashauri nyingine ili kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanaongezeka zaidi. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bi. Rose Robert Manumba amehaidi ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wenzake.
Viongozi wa Wilaya ya Kigoma wakifuatilia mijadara mbaliambali wakati wa Baraza la Madiwani tarehe 4 Novemba 2021.