Halmashauri ina jumla ya barabara 33 zenye mtandao wa urefu wa kilomita 263.5 ambazo zimegawanyika katika maeneo mawili, barabara za wilaya ni kilomita 69.2 na barabara za vijiji kilomita 194.3. kati ya barabara hizi barabara zilizojengwa kwa kiwango cha changarawe zina urefu wa kilomita 29 na barabara zilizojengwa kwa kiwango cha udongo zina urefu wa kilomita 234.5. Aidha sehemu nyingine ya wilaya ni eneo la ziwa Tanganyika ambalo lina takribani ukubwa km 150 na mawasiliano yake ni kwa njia ya meli, boti na Mitumbwi.
Halmashauri imekuwa ikipokea fedha za mfuko wa barabara katika kila mwaka wa fedha kwa ajili matengenezo ya barabara na ujenzi wa makalavati na madaraja. Pamoja na hayo Halmashauri inakabiliwa na changamoto za uhalibifu wa barabara na madaraja hasa kutokana na mvua zinazonyesha, Mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwaka huu iliweza kuharibu madaraja 3 katika barabara ya Bitale – Bubango daraja 2 na Mgarangaza – Mungonya 1.