• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua Pepe za watumishi |
Kigoma District Council
Kigoma District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mkakati
    • Msingi Mkuu
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Elimu Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Afya
      • Huduma za Jamii na Ustawi wa jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • TASAF
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Elimu, afya na maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Orodha ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu ya maombi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Makala
    • Hotuba
    • Machapisho

ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KIGOMA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

Posted on: May 19th, 2022

Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Wilaya ya Kigoma imefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi katika Halmshauri ya Wilaya ya Kigoma. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na maandalizi ya eneo la ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ujenzi wa maabara katika zahanati ya Mahembe iliyopo Kijiji cha Mahembe Kati na ujenzi wa matundu Matano ya vyoo katika zahanati ya Kizenga iliyopo Kijiji cha Kizenga.

Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe (mwenye nguo nyekundu) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma wakikagua maandalizi ya eneo la ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe (kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma akioneshwa mchoro wa jengo la ofisi za Halmashauri zitakazojengwa. Anayemuonesha ni Mhandisi wa kampuni itakayojenga jengo hilo.


Katika kuwasilisha taarifa ya ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba amesema ujenzi huo ni wa jengo la gorofa moja na utafanyika kwa awamu, kiasi cha shilingi Bilioni 3.5 kinatarajiwa kutumika mpaka ujenzi utakapokamilika. Ujenzi huo unafanyika katika kijiji cha Mahembe Kati, Kata ya Mahembe. Akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Kigoma, Mwenyekiti wa Kamati ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe, amesisitiza umakini na usimamizi mzuri wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati. Jengo hilo linajengwa na kampuni iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma akiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma.


Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma pia imetembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na kuangalia kazi ya ujenzi unavyoendelea, Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma amesisitiza juhudi ziongezeke ili mradi ukamilike kwa haraka. 

Pichani juu: Mwonekano wa hatua ya jengo la utawala katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma 

Pichani juu: Mwonekano wa hatua ya jengo la maabara katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma 


Miradi mingine ambayo imetembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma ni ujenzi wa matundu matano ya vyoo katika zahanati ya Kizenga na maabara katika zahanati ya Mahembe. Kamati ya ulinzi imeshauri kuongeza kasi ya ujenzi ili miradi imalizike kwa wakati

Pichani juu: Ukaguzi wa maabara katika zahanati ya Mahembe

Pichani juu: Ukaguzi wa matundu matano ya vyoo katika zahanati ya Kizenga 

Matangazo kwa umma

  • WANAFUNZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 13, 2022
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2022 HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA December 13, 2022
  • TAARIFA KUHUSU HALI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA November 15, 2022
  • TANGAZO LA ZABUNI MBALIMBALI ZA MAPATO YA HALMASHAURI August 30, 2022
  • View All

Habari M-pya

  • MAFUNZO ENDELEVU KAZINI NA SHULE BORA

    December 04, 2022
  • MBIO ZA MWENGE HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

    September 30, 2022
  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA YA WILAYA

    June 29, 2022
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KIGOMA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

    May 19, 2022
  • View All

Video

MAKALA YA MIRADI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
More Videos

Tovuti zinazo fanana

  • Kigoma Ujiji Mc
  • Halmashauri ya Wilaya Uvinza
  • Halmashauri ya Wilaya Buhigwe
  • Halmashauri ya Wilaya Kasulu
  • Halmashauri ya Mji wa Kasulu
  • Halmashauri ya wilaya Kibondo
  • Halmashauri ya wilaya Kakonko

Tovuti Zinazo husiana

  • OFISI YA RAIS TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI (NECTA)
  • WIZARA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • MKOA WA KIGOMA
  • TOVUTI YA TAIFA
  • MFUMO WA MADENI YA WATUMISHI SERIKALINI
  • SALARY SLIP PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR

    Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA

    Telephone: 028 2804865

    Mobile: 028 2804865

    Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Usiri
    • Vigezo
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 H/W Kigoma . Haki zote zimehifadhiwa