Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umekimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma tarehe 21/08/2023, ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe. Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma umekagua na kufungua miradi ya maendeleo 5 yenye thamani ya shilingi 1,943,835,587, ambayo ni Ujenzi wa Kituo cha Afya Kalinzi-shilingi 500,000,000, Kikundi cha Miche ya Kahawa Kalinzi - shilingi 750,000,000, Kikundi cha Uwekezaji Wanawake Kiuchumi (Mwakeye) Mkigo - shilingi 12,000,000, Ujenzi wa vyumba vya 4 vya madarasa na vyoo Matundu 3 katika Shule ya Msingi Kidahwe shilingi 110,600,000 na mradi wa barabara yenye kilomita 0.5 Mwandiga shilingi 571,235,587. Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Ngd. Abdalla Shaib Kaim amesisitiza miradi kujengwa kwa ubora ili thamani ya pesa pesa ionekane.
Pichani juu: Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2023 akisalimiana na Kamati ya Ulinzi ya Halmashaurir ya Wilaya ya Kigoma
Pichani juu: Watumishi wa Wilaya ya Kigoma katika mapokezi ya Mwenge Wilaya ya Kigoma
Pichani juu: Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023 wakikagua nyaraka za ujenzi katika Kituo cha afya Kalinzi.
Pichani juu: Uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha afya Kalinzi
Pichani juu: Ushiriki wa usafi soko la Mkongoro wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Pichani juu: Vyumba vya 4 vya madarasa vimefunguliwa na Mwenge wa Uhuru 2023.
THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR
Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA
Telephone: 028 2804865
Mobile: 028 2804865
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Kigoma . Haki zote zimehifadhiwa