Mkutano wa kwanza wa Baraza la Halmashauri wa tarehe 15 Desemba 2020 ulifanyika kwa Waheshimiwa Madiwani kuanza kuapa kisha kufuatiwa na uchaguzi wa Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Mkutano wa kwanza wa Baraza ulimchagua Diwani wa kata ya Kagunga Mh. Joseph Nyambwe kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020-2025 na Mh. Albogast Ndiyuze Diwani wa kata ya Bitale alichaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Mkutano wa kwanza wa Baraza uliunda Kamati za kudumu za Halmashauri na kupitisha ratiba ya vikao. Mkutano wa kwanza wa Baraza pia ulipokea taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu kumbukumbu ya maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizofanyika katika kipindi ambacho Baraza la Madiwani lilivunjwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Samson Anga (aliyesimama) akisalimia na kutoa neno kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la Halmashauri wa tarehe 15 Desemba 2020.
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti akitoa maelekezo kabla ya uchaguzi.
Mh. Assa N. Makanika Mbunge wa Jimbo ya Kigoma Kaskazini akifuatilia kwa makini mkutano wa kwanza wa Baraza la Halmashauri wa tarehe 15 Desemba 2020.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza wakishangilia na kucheza baada ya kushuhudia viapo kwa Madiwani wateule wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR
Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA
Telephone: 028 2804865
Mobile: 028 2804865
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Kigoma . Haki zote zimehifadhiwa