• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua Pepe za watumishi |
Kigoma District Council
Kigoma District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mkakati
    • Msingi Mkuu
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Elimu Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Afya
      • Huduma za Jamii na Ustawi wa jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • TASAF
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Elimu, afya na maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Orodha ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu ya maombi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Makala
    • Hotuba
    • Machapisho

MIKOPO YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 122 YATOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

Posted on: March 30th, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma inaendelea kutenga na kupeleka mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na vikundi vya watu wenye ulemavu kwa mujibu wa sheria na kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo. Mikopo hii inatokana na asilimia 10 ya Mapato ya ndani yanayokusanywa na Halmashauri kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato. Taarifa iliyosomwa na Afisa Maendeleo  ya Jamii Bi. Minza Edward mbele ya Mgeni rasmi Mh. Salum Hamisi Kalli ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, imesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imefanikiwa kutenga na kupeleka mikopo kiasi cha shilingi 122,492,583 kwa vikundi 11 ambapo vikundi vya wanawake 4, vijana 4 na vikundi vya watu wenye ulemavu 3. Aidha kiasi cha shilingi 45,514,583 zimetokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya mwezi Julai 2022 hadi Januari 2023 na kiasi cha shilingi 76,978,000 ni fedha zinazotokana na marejesho ya mikopo iliyokopeshwa miaka ya nyuma. 

Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Hamisi Kalli (mwenye Suti Nyeusi) aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla ya utoaji mikopo.


Pichani juu: Mfano wa Hundi ya shilingi Milioni 122,492,583 iliyotolewa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.


Pichani juu: Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Hamisi Kalli (mwenye Suti Nyeusi) akikabidhi cheti kwa mmoja wa kiongozi wa kikundi vijana.


Pichani juu: Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Hamisi Kalli (mwenye Suti Nyeusi) akikabidhi cheti kwa mmoja wa kiongozi wa kikundi cha wanawake.


Akiongea katika hafla hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Hamisi Kalli amewasisitiza wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia mikopo katika shughuli iliyokusudiwa na kikundi. Mgeni rasmi pia amesisitiza vikundi hivyo kufanya marejesho ya mikopo hiyo ili na wananchi wengine pia wanufaike.

Vikundi hivyo vinajishughulisha na biashara ya mazao ya nafaka, biashara ya Mawese, Ufugaji wa kuku na mbuzi, utengenezaji wa sabuni, mashine ya kusaga, biashara ya samaki na dagaa na kiwanda kidogo cha utengenezaji wa chaki. 

Pichani juu: Ni baadhi ya wakuu wa idara na vitengo pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Hamisi Kalli (aliyekaa mwenye Suti Nyeusi)


Pichani juu: Afisa Maendeleo Bi. Minza Edward (kushoto aliyesimama) akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Mh. Salum Hamisi Kalli, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma


Pichani juu: Ni vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wakimsikiliza mgeni rasmi.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ndugu. Jabir Timbako amesema wataendelea kutenga pesa na kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa mujibu wa sheria na kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo hiyo. 

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mh. Albogast Ndiyuze amesisitiza lengo la mikopo hii ni kuwainua wananchi kiuchumi. Amesema mikopo hii ni sehemu ya kile ambacho tumekusanya kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato na ikiwemo ushuru wa biashara zinazofanywa na wananchi hao.

Hafla hiyo ya utoaji mikopo imehudhuliwa pia na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambaye amewakilishwa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)

Matangazo kwa umma

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II March 13, 2023
  • WANAFUNZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 13, 2022
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2022 HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA December 13, 2022
  • TAARIFA KUHUSU HALI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA November 15, 2022
  • View All

Habari M-pya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA YAFANYA KIKAO CHA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE

    May 12, 2023
  • MKUU WA WILAYA YA KIGOMA AFANYA ZIARA KATIKA KATA YA KAGUNGA

    May 07, 2023
  • MIKOPO YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 122 YATOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    March 30, 2023
  • MEMKWA KUSAIDIA WALIOKOSA ELIMU KWA MFUMO RASMI

    March 21, 2023
  • View All

Video

MAKALA YA MIRADI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
More Videos

Tovuti zinazo fanana

  • Kigoma Ujiji Mc
  • Halmashauri ya Wilaya Uvinza
  • Halmashauri ya Wilaya Buhigwe
  • Halmashauri ya Wilaya Kasulu
  • Halmashauri ya Mji wa Kasulu
  • Halmashauri ya wilaya Kibondo
  • Halmashauri ya wilaya Kakonko

Tovuti Zinazo husiana

  • OFISI YA RAIS TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI (NECTA)
  • WIZARA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • MKOA WA KIGOMA
  • TOVUTI YA TAIFA
  • MFUMO WA MADENI YA WATUMISHI SERIKALINI
  • SALARY SLIP PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR

    Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA

    Telephone: 028 2804865

    Mobile: 028 2804865

    Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Usiri
    • Vigezo
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 H/W Kigoma . Haki zote zimehifadhiwa