Kusimamia na kujenga miradi ya maji na kuhakikisha huduma ya maji inatolewa kama ilivyokusudiwa.
Kuunda na kusimamia Jumuiya za watumiaji maji (Cowsos) kwa ajili ya uendeshaji wa miradi ya maji kwa mujibu wa sera ya maji ya 2009 inayotaja ushirikishwaji wa wananchi katika uendeshaji wa miradi ya maji.
Kuhakikisha huduma ya maji inakuwa endelevu katika vijiji vyote ambavyo vina miradi ya maji.
Kutoa elimu ya utunzaji wa vyazo vya maji na mazingira yanayozunguka vyanzo hivyo.
Kuandaa usanifu wa miradi mipya ya maji na kufanya ukarabati wa miradi iliyochakaa.